Loading...

Msiba wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC, Etienne Tshisekedi waibua mvutano mkubwa

MIPANGO ya kurudisha mwili wa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Etienne Tshisekedi kutoka Brussels, Ubelgiji hadi mjini Kinshasa kwa mazishi, imesababisha serikali na chama chake kutofautiana.

Serikali ya DRC imeahidi kuruhusu jeneza lake kupelekwa bungeni na pia kusema kuwa itawalipia ndege waliokuwa wanasiasa wenzake hadi Ubelgiji kuuchukua mwili huo.

Hata hivyo, chama cha Tshisekedi cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), kimekataa pendekezo hilo na badala yake kutangaza masharti yake.

Chama hicho kilisema serikali inastahili kumjengea makumbusho Tshisekedi katikati ya mji wa Kinshasa na pia kimetaka gharama ya mazishi kulipwa na serikali inayokuja ambayo muundo wake umeafikiwa, ingawa bado haijaingia madarakani.

Maafikiano ya kubuniwa serikali mpya inayojumuisha muungano wa upinzani uliobuniwa na Tshisekedi ilikuwa na sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana.

Serikali imejibu masharti ya UDPS ya kujengwa kwa makumbusho, lakini imesema kuwa haitajengwa katikati ya mji.
Msiba wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC, Etienne Tshisekedi waibua mvutano mkubwa Msiba wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC, Etienne Tshisekedi waibua mvutano mkubwa Reviewed by Zero Degree on 2/11/2017 03:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.