Loading...

VIDEO: Bunge lakemea wabunge kukamatwa kibabe

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekemea tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.

Akihitimisha mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa serikali anamhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda kibabe kumkamata.

“Kama kuna afisa yeyote anayemuhitaji mbunge lazima aniambie kwanza hatuwezi kwenda hivyo, kwa hakika tukienda hivi kibabe kibabe namna hii tutaivuruga nchi,” alisema Spika huyo.

Aidha Spika Ndugai amewatoa hofu wabunge kuhusu hadhi ya Bunge na kusema kuwa hadhi ya chombo hicho haijashuka, na kwamba mhimili huo hauna mgogoro wowote na serikali wala mahakama.

Mheshimiwa Ndugai alisema hayo kufuatia malalamiko ya wabunge wa upinzani yaliyotolewa hivi karibuni juu ya utaratibu unaotumiwa na Jeshi la Polisi kukamata wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge, wakitolewa mfano wabunge Tundu Lissu na Godbless Lema.


VIDEO: Bunge lakemea wabunge kukamatwa kibabe VIDEO: Bunge lakemea wabunge kukamatwa kibabe Reviewed by Zero Degree on 2/11/2017 03:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.