Loading...

Mwisho wa enzi za Wenger Arsenal, wakongwe waendelea kumkomalia ang'oke kikosini

Siku zinavyozidi kwenda hali ya Arsene Wenger ndani ya Arsenal inazidi kuwa ya sintofahamu. Mashabiki wanaonekana kuchoshwa na Mfaransa huyo na kuanza kuonesha hisia zao waziwazi. Mbaya zaidi ni habari za Arsenal kuandaa mkataba mpya wa miaka miwili na Arsene Wenger.

Tayari watu wengi wameanza kuongea mengi kuhusu Wenger lakini leo tunakuletea maoni ya baadhi ya wachezaji wa zamani wa Arsenal.

Alan Smith mchezaji wa zamani wa Arsenal ambae amewahi kushinda makombe matano na Arsenal.Smith alishinda makombe hayo kabla ya ujio wa Wenger na sasa ana yake kuhusu Wenger.Smith anaamini ni wakati sahihi sasa wa Arsene Wenger kuondoka.

Smith amesema “kila siku mashabiki wasiokuwa na furaha wanaongezeka,kelele za kutokuwa na furaha zimezungumziwa kwa miaka 20 sasa ni muda mrefu na nadhani ni wakati sahihi wa timy kutafuta kocha mwingine”.Smith anaona mmiliki wa timu hiyo Stan Kroenke hapaswi kuridhika tu na kufuzu nafasi ya nne kila msimu bali anapaswa kutazama kitu kipya klabuni hapo.

Naye Andy Smudge ambae katika mechi 347 alizochezea Arsenal alifanikiwa kuifungia magoli 115 haamini kama Wenger atasaini mkataba mpya. Pamoja na Arsenal kupanga kumpa mkataba mpya Wenger lakini Smudge anaamini Wenger anaweza kuukataa mkataba huo na kuendelea na mambo mengine. Smudge anaamini Arsenal wanawaumiza sana mashabiki wao. Anawaonea huruma mashabiki ambao hutumia pesa nyingi lakini mwisho matokeo ya timu huwa ni mabovu.

Thiery Henry
yeye hakutaka kumpa mzigo mkubwa Wenger. Henry anaona tatizo la Arsenal sio Wenger pekee bali hata wachezaji pia. Henry anasema Wenger ameiongoza Arsenal vyema japo kwa sasa naye hayuko upande wake. ”Tusahau yote ya nyuma lakini kwa sasa kushiriki ligi misimu 12 bila kombe ni jambo baya” alisema Henry.Kuhusu wachezaji Henry alisema “wanahitaji kupambana kila muda, wana wachezaji wakubwa na wazuri lakini wanakosa kujiamini”

Naye Ian Wright nguli wa zamani wa Arsenal amedai ameshapata taarifa kwamba Wenger anaondoka. Wright alisema Wenger alimuambia mwenyewe kwamba anakaribia kuondoka. “Aliniambia mwisho umekaribia, sijawahi kumskia akisema neno kama hilo hapo kabla lakini naamini sasa hili linaenda kutokea”
Mwisho wa enzi za Wenger Arsenal, wakongwe waendelea kumkomalia ang'oke kikosini Mwisho wa enzi za Wenger Arsenal, wakongwe waendelea kumkomalia ang'oke kikosini Reviewed by Zero Degree on 2/13/2017 01:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.