Loading...

47 wanashikiliwa na Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Watu 47 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani kilimanjaro kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Bangi na Mirungi kutoka ndani na nje ya nchi.

Kamanda wa pilisi mkoa wa Kilimanjaro SACP. Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na misokoto 269 ya bangi na mirungi kilo 32.

Aidha kamanda mutafungwa amesema kwa sasa wasafirishaji wa madawa hayo wamebuni mbinu mpya ya kupulizia marashai mabegi yaliyobeba madawa hayo kupeleka mikoani ili wasijulikane.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Said Meck Sadick amesema operesheni hiyo ni endelevu na kwamba kwa sasa kuina taarifa za uwepo wa wafanaybiasha waliokimbia Dar es Salaam kuja Kilimanjaro kuendeleza biashara ya kusafirisha dawa hizo kupitia njia za panya.

Naye kamishna mkuu wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Bw.Rogus Willium Sianga serikali imeanza kuchukua hatua za kuwashughulikia wafanyabiashara wanaotumia akina mama wanaofanyabiashara ndogondogo katika wilaya ya rombo kusafirisha madawa ya kulevya kupitia mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Kitobo ambalo ndyo njia maarufu wanayotumia kupitishia madawa hayo.

Source: ITV
47 wanashikiliwa na Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. 47 wanashikiliwa na Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. Reviewed by Zero Degree on 2/13/2017 01:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.