Loading...

Rais Adama Barrow amemfukuza kazi mkuu wa majeshi nchini Gambia

Aliyekuwa mkuu wa majeshi Gambia, Jenerali Ousman Badjie
Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie.

Jenerali Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.

Jenerali Ousman Badjie
Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana.

Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.
Rais Adama Barrow amemfukuza kazi mkuu wa majeshi nchini Gambia Rais Adama Barrow amemfukuza kazi mkuu wa majeshi nchini Gambia Reviewed by Zero Degree on 2/28/2017 09:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.