Loading...

Real Madrid yaingia vitani dhidi ya Chelsea katika kusaka saini ya nyota huyu

Real Madrid wako tayari kwa upinzani wa aina yoyote ile na klabu ya Chelsea katika kusaka saini ya nyota wa Celtic, Moussa Dembele.

Dembele amekuwa ni moto wa kuotea bali nchini Scotland tangu aliposajiliwa akitokea Fulham msimu uliopita.


Kiwango chake kwa sasa kimezivutia baadhi ya klabu bora za Ulaya. Fomu yake ilikuwa imfanye asajiliwe na Chelsea katika tarehe za mwisho za usajili, lakini kamwe haiukutokea.

Sasa, Chelsea inaweza kuwa na nafasi ndogo ya kumsajili nyota huyo kwani Real Madrid nao pia wako katika harkati za kumnasa mchezaji huyo.



Celtic wamefanya tathmini yao juu ya mchezaji huyo na kumuweka katika viwango vya ada ya uhamisho ya pauni milioni 40, kiasi ambacho Real Madrid itakuwa tayari zaidi kulipa mapema iwezekanavyo.

Ukiziacha klabu za Chelsea na Real Madrid, ukienda ujerumani katika klabu za Bayern Munich na RB Leipzig wote pia wamekuwa kiu ya kumsajili Dembele mwishoni mwa msimu.

Real Madrid yaingia vitani dhidi ya Chelsea katika kusaka saini ya nyota huyu Real Madrid yaingia vitani dhidi ya Chelsea katika kusaka saini ya nyota huyu Reviewed by Zero Degree on 2/20/2017 01:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.