Sababu ambazo zitaimaliza Yanga alizozitaja Kocha Joseph Omog ziko hapa
KIU ya kucheza mashindano ya kimataifa na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiyo sababu kuu mbili zitakazoifanya Simba iibuke na ushindi katika mechi dhidi ya watani zao Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, watani hao wa jadi walitoka sare ya bao 1-1 lakini Simba wataingia uwanjani wakiwa ndiyo vinara kwenye msimamo wa ligi.
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema kuwa amekiandaa kikosi chake kucheza kwa umakini na tahadhari ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.
Omog alisema mechi ya Jumamosi si ngumu kutokana na timu pamoja na wachezaji wote kufahamiana.
"Wanajuwa ugumu na udhaifu wa kila mmoja wao, ni mechi ambayo tunatakiwa kuongeza umakini, kutumia vyema nafasi na kutoruhusu mashambulizi upande wetu," alisema kocha huyo aliyeipa ubingwa wa Bara timu ya Azam FC msimu wa 2013/14.
Aliongeza kuwa kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali na hiyo inawafanya wachezaji wake wajiandae kuonyesha uwezo katika dakika zote 90.
"Nafurahi kuona hata mazoezini kila mchezaji amebadilika, wanajituma zaidi kwa sababu wanataka kupata nafasi ya kucheza na kuisaidia timu kupata pointi tatu, tumejipanga kupambana kwa sababu tunahitaji kushinda tu, hakuna zaidi ya hilo," Omog alisema.
Wakati huo huo, meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan 'Mgosi' alisema kuwa beki wao Method Mwanjali anaendelea na mazoezi na wachezaji wenzake na hatima ya kucheza katika mchezo huo wa Jumamosi itajulikana keshokutwa.
Source: Nipashe

Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2017 01:39:00 PM
Rating: