BREAKING NEWS: Raisi Magufuli AMSIMAMISHA KAZI Mkurugenzi wa jiji la Dar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza kumfuta kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe.
Hatua ya kumfuta kazi Mkurugenzi huyo imefuata baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kumwambia Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, kuwa Mkurugenzi huyo wa Jiji alisaini mikataba kadhaa ambapo mmoja kati ya hiyo wa tozo za mabasi ya abiria ya kwenda mikoani imelisababishia taifa hasara ya shilingi takribani bilioni 3, ambapo kwa kila mwezi zilikuwa zinapotea shilingi milioni 42 tangu 2015- 2016.
“Jamani Mnataka mimi nifanyeje?, Mnataka nitumbue Jipu hapa hapa? Wangapi wanataka nitumbue? Basi kwa vile umezungumza wewe Mkuu wa Mkoa, na mimi niliapa kusimamia sheria, na mimi viongozi wa namna hii hii ambao wanafaidi jasho la watu masikini, kwenye Serikali yangu hawana Nafasi, Kwahiyo kuanzia sasa kabwe nime msimamisha kazi, Nendeni mkajulishe hivo, na hata ile miradi imesimamishwa kazi, Sitakuwa na Simile, Pakitokea Jipu sisubiri maana litaota usaa” Alisema Rais Magufuli
Unaweza kuisikiliza hapo chini Sauti wakati Rais Magufuli akitangaza kumfuta kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
RAIS MAGUFULI : "NILIKATAA DARAJA LA KIGAMBONI KUPEWA JINA LANGU..."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, leo amezindua Daraja la Kigambini na kulipa jina la Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa heshima ya Taifa la Tanzania.
Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amesema alikataa ombi la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kuliita daraja hilo jina la Rais Magufuli na badala yake ameamua kuliita Daraja la Nyerere kwa heshima ya Baba wa Taifa kwa mema aliyoyafanya katika nchi hii.
“Waziri wa Ujenzi aliponifata na kuniambia daraja hili lipewe jina langu nilikataa kwa sababu mawazo ya kulijenga yalianza tangu enzi za Baba wa Taifa, kama yapo niliyoyafanya nilikuwa natimiza wajibu wangu sistahili sifa yoyote … kama mtaniruhusu ndugu zangu daraja hili tuliite Daraja la Nyerere” amesema Rais Magufuli.
Amesema Tanzania imepiga hatua kwa kipindi kifupi kwa kujenga madaraja makubwa yanayounganisha mikoa ya Tanzania na nchi za jirani ambayo ni Daraja la Mkapa, Kikwete, Umoja na mengine yanayoendelea kujengwa.
Mapema leo Rais Dk. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo limefanyika mapema leo asubuhi kabla ya Rais kwenda kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa Daraja la Kigamboni Jijini hapa.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Balozi Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.
ZeroDegree.
BREAKING NEWS: Raisi Magufuli AMSIMAMISHA KAZI Mkurugenzi wa jiji la Dar
Reviewed by Zero Degree
on
4/19/2016 06:02:00 PM
Rating: