Loading...

Daraja la Kigamboni lazinduliwa rasmi leo.



Muonekano wa daraja la kigamboni.

Uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam wafanyika leo Aprili 19, 2016




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. (PICHA ZOTE NA IKULU)

RAIS wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Magufuli leo amezindua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 ambalo limejengwa juu ya Bahari ya Hindi kuunganisha kata za Kigamboni na Kivukoni.

Katika hafla ya uzinduzi huo, rais Magufuli amesema kuwa, daraja hilo lisiitwe ‘Daraja la Magufuli’ na badala yake amependekeza lipewe jina la muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyewaunganisha Watanzania bila kujali itikadi ya vyama, dini, kabila wala rangi.

Akiongea wakati wa kuzindua daraja hilo leo, Rais Magufuli amesema kuwa awali aliletewa mapendekezo na waziri mwenye dhamana akimtaka aridhie daraja hilo lipewe jina lake, lakini kwakuwa wazo la ujenzi huo lilianza tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, alikataa na kushauri jina la Nyerere litumike.

“Nilikataa lisiitwe kwa jina langu kwa sababu wazo la ujenzi wa daraja hili lilianza mwaka 1979 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

“Wazo hilo halikufanikiwa kutokana na ukosefu wa pesa wakati huo. Mwalimu Nyerere ni kiongozi aliyejenga misingi imara katika taifa letu.

“Alikuwa ni kiongozi asiyebagua mtu kwa misingi ya dini, chama au kabila. Alifanikiwa kutuunganisha watanzania wote bila kujali itikadi zetu.

“Leo hii, daraja hili limekamilika, ni daraja ambalo halitambagua mtu kwa sababu wa CCM watapita hapa, wa Chadema watapita hapa na bahati nzuri mstahiki Meya wa jiji hili ambaye ni Chadema naye yuko hapa na amepita katika daraja hili.

“Ndugu zangu sistahili sifa zozote, najua nimefanikisha ujenzi huu nikiwa waziri wa ujenzi, lakini wakati huo nilikuwa natimiza wajibu wangu kama mtumishi wa umma, hivyo nashauri hili daraja liitwe daraja la Nyerere ili tuweze kumuenzi mwasisi wa taifa hili” alisema Rais Magufuli.

Mbali na hilo, rais Magufuli pia hakusita kuzungumzia suala la kulipisha wananchi watakaokuwa wanavuka kwa kutumia daraja hilo na kusema kuwa, watakaopita kwa gari, pikipiki na baiskeli lazima walipie (jpo hakutaja kiwango watakachotakiwa kulipia) na kwamba wataendelea kulipia mpaka pale ambapo tamko jingine utakapotolewa wakati huo waenda kwa miguu hawatalipia, watapita bure. Akaongeza kuwa tozo hiyo itasaidia kuongeza kipato kitakachotumika kujenga daraja lingine kama hilo.

Daraja la Kigamboni limejengwa katika mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek), mradi huu uliobuniwa na Arab Consulting Engineers na kujengwa na wakandarasi kampuni za China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company, unamilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Aidha Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa Taifa.





ZeroDegree.
Daraja la Kigamboni lazinduliwa rasmi leo. Daraja la Kigamboni lazinduliwa rasmi leo. Reviewed by Zero Degree on 4/19/2016 05:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.