Loading...

Siku 15 ngumu kwa Kocha Jose Mourinho Machester United

KOCHA, Jose Mourinho ana wakati mgumu wa kuhakikisha mastaa wake pumzi hazikati baada ya kukabiliwa na mechi tano za nguvu ndani ya siku 15 kuanzia jana Jumamosi.

Manchester United inakabiliwa na mechi tano muhimu sana ndani ya siku hizo 15 jambo linalomfanya kocha Mourinho kuhakikisha anasimamia vyema vipindi vyote vya mazoezi kwa umakini ili kusiwepo na majeruhi ambao watapunguza ukubwa wa kikosi jambo litakalowafanya wawe kwenye wakati mgumu. Kwenye mechi hiyo, Man United itakabiliwa na fainali ya Kombe la Ligi na mtoano wa Europa League.

Hapo hapo kutakuwa na mechi ya mtoano pia kwenye Kombe la FA dhidi ya Blackburn Rovers na awali ilipaswa kucheza mechi mbili za Ligi Kuu, ikiwamo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchester, Manchester City, lakini sasa imeahirishwa kwa sababu siku hiyo watakipiga na Southampton uwanjani Wembley kwenye fainali ya Kombe la Ligi.

Kutokana na hilo, Mourinho amepanga kutowafanyisha wachezaji wake mazoezi magumu sana ili kuwafanya kupumzika na kuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha wanashinda mechi. Kocha huyo hataki kufanya makosa katika vita ya kuwania nafasi ya nne.
Siku 15 ngumu kwa Kocha Jose Mourinho Machester United Siku 15 ngumu kwa Kocha Jose Mourinho Machester United Reviewed by Zero Degree on 2/12/2017 01:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.