Loading...

Umoja wa Afrika [AU] kujiondoa katika mahakama ya kimataifa ICC

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika katika kikao chao katika makao makuu ya Umoja wa Afrika AU
Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.

Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.

Viongozi wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Jengo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki za binaadamu.
Umoja wa Afrika [AU] kujiondoa katika mahakama ya kimataifa ICC Umoja wa Afrika [AU] kujiondoa katika mahakama ya kimataifa ICC Reviewed by Zero Degree on 2/01/2017 12:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.