Loading...

VIDEO: KRC Genk ya Samatta yafanikiwa kuingia hatua ya 16 bora Europa League

Mbwana Samatta ameandika historia nyingine tena usikuwa wa Alhamisi February 24, 2017 baada ya timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League.

Genk wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena, wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Astra Giurgiu ya Romania na kuiondosha kwenye mashindano hayo kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya michezo miwili.

Mchezo wa awali uliopigwa juma lililopita (February 16, 2017) , Genk ililazimisha sare ya kufunga 2-2 ugenini na kujiweka kwenye nafasi nzuri kwa faida ya magoli ya ugenini.

Goli pekee kwenye mchezo wa marudiano limefungwa na Alejandro Pozuelo dakika ya 67 kipindi cha pili kwa free-kick iliyozama moja kwa moja wavuni.


VIDEO: KRC Genk ya Samatta yafanikiwa kuingia hatua ya 16 bora Europa League VIDEO: KRC Genk ya Samatta yafanikiwa kuingia hatua ya 16 bora Europa League Reviewed by Zero Degree on 2/24/2017 10:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.