Loading...

VIDEO: Man U yasonga mbele kwenye ligi ya Europa baada ya kushinda mechi zote mbili, nyumbani na ugenini

Manchester United walifika hatua ya 16 bora katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Saint-Etienne Jumatano.

Hata hivyo, mfungaji wa goli la Manchester Henrikh Mkhitaryan huenda akakosa mechi ya Kombe la EFL Jumapili baada ya kuumia na kulazimika kuondoka uwanjani wakati wa mechi hiyo.

United walikuwa mbele 3-0 kutokana na ushindi wa mechi ya kwanza, mabao yote yakitoka kwa Zlatan Ibrahimovic.

Kwenye mechi ya Jumatano iliyochezewa Ufaransa, Mkhitaryan alifunga dakika ya 16 kupitia krosi iliyotoka kwa Juan Mata.



Muda mfupi baadaye hata hivyo, mchezaji huyo kutoka Armenia alionekana kuumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka wuwanjani.

Beki wao Eric Bailly pia alifukuzwa uwanjani dakika ya 63 baada ya kuonesha kadi ya pili ya njano.
VIDEO: Man U yasonga mbele kwenye ligi ya Europa baada ya kushinda mechi zote mbili, nyumbani na ugenini VIDEO: Man U yasonga mbele kwenye ligi ya Europa baada ya kushinda mechi zote mbili, nyumbani na ugenini Reviewed by Zero Degree on 2/23/2017 12:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.