Loading...

Vurugu zaendelea kutawala bungeni, Afrika kusini kumpinga Rais Zuma

Wanachama wa chama cha EFF wakikabiliana na walinda usalama wakati wa hotuba ya Rais mwaka 2015
Bunge la Afrika kusini jana lilijawa na vurugu kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.

Polisi wakituliza ghasia nje ya Bunge la Afrika kusini
Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala.

Awali nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza kuwasambaratisha.

Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hutuba yake.
Vurugu zaendelea kutawala bungeni, Afrika kusini kumpinga Rais Zuma Vurugu zaendelea kutawala bungeni, Afrika kusini kumpinga Rais Zuma Reviewed by Zero Degree on 2/10/2017 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.