Loading...

Waziri Lukuvi kumchukulia hatua mfanyabiashara aliyempa Paul Makonda shamba

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake ni mali ya Serikali.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo Jumatatu hii katika mkutano wake na wanahabari. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,” amesema Lukuvi

Aidha Lukuvi amesema anataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya wa ajili ya uhakiki.

Source: Mwananchi
Waziri Lukuvi kumchukulia hatua mfanyabiashara aliyempa Paul Makonda shamba Waziri Lukuvi kumchukulia hatua mfanyabiashara aliyempa Paul Makonda shamba Reviewed by Zero Degree on 2/27/2017 03:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.