Loading...

Wenger asema hajakata tamaa ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza [EPL]

Arsenal ni sharti iamini kwamba bado inaweza kushinda ligi ya Uingereza msimu huu licha ya pengo la pointi 12 kati yake na viongozi wa ligi Chelsea ,kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.

The Gunners, ambao kwa mara ya mwisho walishinda ligi mwaka 2004 walishuka hadi nafasi ya 4 baada ya kushindwa 3-1 na Chelsea Jumamosi iliopita.

Kikosi cha Wenger kinaialika Hull City katika uwanja wa Emirates baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa ilizocheza.

''Bado hatujasalimu amri'', alisema raia huyo wa Ufaransa.''Hata iwapo unadhani tumeshafanya hivyo, mimi bado sijasalimu amri-hatuweza kufikiria hivyo''.

Kwa sasa ni pointi tano pekee zinazotutenganisha na Tottenham ilio nafasi ya pili na Manchester United iliyopo katika nafasi ya sita.

Aliongezea Wenger: Tuko katika eneo ambalo ni gumu sana na ugombeaji wa kila nafasi ni muhimu sana msimu huu ikilinganishwa na ule uliopita.
Wenger asema hajakata tamaa ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] Wenger asema hajakata tamaa ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza [EPL] Reviewed by Zero Degree on 2/09/2017 05:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.