Loading...

Ajeruhi watu zaidi ya wanne kwa kisu kabla ya kupigwa risasi na kufariki papo hapo mkoani Singida

Mkazi mmoja wa ikungi mkoani singida amepigwa risasi na kufariki papo hapo ,baada ya kuwajeruhi kwa kisu watu zaidi ya wanne akiwemo mke wake na kuhatarisha maisha ya askari polisi wanne kwa kutaka kuwachoma kisu wakati wakitaka kumkamata.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba,amemtaja aliye pigwa risasi na kufariki marehemu Herman Joseph miaka thelasini na mbili mkazi wa Ikungi madukani, baada ya kubishana na mke wake alitoa kisu na kumchoma makalioni , na watu walipo fika kutoa msaada aliwachoma kisu watu wengine watatu.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya skari kufika marehemu Herman alifanya jaribio mara mbili la kutaka kuwachoma kisu askari licha ya askari kupiga risasi hewani ,lakini askari mmoja katika jitihada za kukwepa kisu alianguka na maremu kumlalia askari huyo kwa kutaka kumchoma kisu kifuani,ndipo alipo fyatua risasi kwa kuokoa maisha yake na wengine na kusababisha kifo.

Kutokana na tukio hilo la marehemu kuchoma watu visu kamanda Mgiligimba alipoulizwa na ITV alisema kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya akili ambayo huwa yana tokea na muda mwingine ana kuwa katika hali ya kawaida,pia amesema jeshi lake bado lina endelea na uchunguzi zaidi kubaini ukweli wa tukio hilo.

Source: ITV
Ajeruhi watu zaidi ya wanne kwa kisu kabla ya kupigwa risasi na kufariki papo hapo mkoani Singida Ajeruhi watu zaidi ya wanne kwa kisu kabla ya kupigwa risasi na kufariki papo hapo mkoani Singida Reviewed by Zero Degree on 3/16/2017 12:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.