Aliyeingia Ikulu ya Marekani kwa kuruka ukuta anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela
MWANAMUME mmoja aliyekuwa amebeba mkoba na kuingia Ikulu ya Marekani kwa kuruka ukuta, alikamatwa juzi na maofisa wa usalama.
Kosa hilo ni la kuhatarisha usalama wa nyumba ya rais wa Marekani.
Rais Donald Trump alikuwamo ndani wakati Jonathan Tran mwenye umri wa miaka 26 aliporuka ukuta wa saa 5:38 usiku.
Taarifa ya maofisa wa usalama ilisema Tran alikamatwa na wanasalama wenye nguo za raia. Tran mkazi wa California anashikiliwa bila dhamana.
Raisi Trump aliwashukuru maofisa wa usalama kwa kumtia mbaroni kijana huyo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa ofisi ya Mwanasheria Kuu wa Marekani, Bill Miller, Tran anashitakiwa kwa kuingia eneo ambalo mtu harusiwi akiwa amebeba silaha ya hatari, na anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.
Rais Donald Trump alikuwamo ndani wakati Jonathan Tran mwenye umri wa miaka 26 aliporuka ukuta wa saa 5:38 usiku.
Taarifa ya maofisa wa usalama ilisema Tran alikamatwa na wanasalama wenye nguo za raia. Tran mkazi wa California anashikiliwa bila dhamana.
Raisi Trump aliwashukuru maofisa wa usalama kwa kumtia mbaroni kijana huyo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa ofisi ya Mwanasheria Kuu wa Marekani, Bill Miller, Tran anashitakiwa kwa kuingia eneo ambalo mtu harusiwi akiwa amebeba silaha ya hatari, na anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.
Aliyeingia Ikulu ya Marekani kwa kuruka ukuta anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela
Reviewed by Zero Degree
on
3/13/2017 11:40:00 AM
Rating: