Loading...

Bara la Africa sasa lapata anwani yake ya matandao '.africa' sawa na '.com'

Bara la Afrika sasa lina anwani yake ya mtandao .africa sawa na ule wa .com kufuatia uzinduzi wake rasmi na muungano wa Afrika AU.

Mwenyekiti wa tume ya umoja huo Nkoszana Dlamini alipongeza uzinduzi wake kama wakati ambapo Afrika imejipatia utambulisho wake wa kidijitali.

Bara la Afrika sasa lina anwani yake ya mtandao
AU inasema kuwa anwani ya .africa utalileta pamoja bara la Afrika kama jamii ya mtandao.

Anwani hiyo sasa itaonyesha maslahi ya makampuni barani Afrika.

Kwa mfano kampuni ya simu inaweza kuanzisha anwani yake ya mobile.africa ili kuonyesha uwepo wake barani Afrika.

Icann, kampuni inayotengeza anwani hizo iliiidhinisha hatua hiyo baada ya AU kuwasilisha ombi.

Kampuni hiyo iliongozwa na kampuni ya Afrika Kusini ZA Central Registry ambayo itahusika na usajili wa majina ya .africa.

Source: BBC Swahili
Bara la Africa sasa lapata anwani yake ya matandao '.africa' sawa na '.com' Bara la Africa sasa lapata anwani yake ya matandao '.africa' sawa na '.com' Reviewed by Zero Degree on 3/12/2017 01:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.