Loading...

Brazil ndio taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018

Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezewa nchini Urusi mwaka ujao.

Walifuzu baada ya kuilaza Paraguay kwa magoli 3-0, wakati huo huo Argentina na Uruguay wakipoteza pointi 3.

Brazil wamefunga mabao 24 na kufungwa mawili pekee mechi zao nane za karibuni za kimataifa
Hii ina maana kwamba, Brazil hawataweza kumaliza chini ya nafasi nne bora miongoni mwa mataifa ya Amerika Kusini, ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo yatakayofuzu.



Brazil waliilaza Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.

Neymar pia alipoteza mkwaju wa penalti.

Brazil kwa sasa wanaongoza kwa pointi 9 mbele ya Colombia ambao wanashikilia nafasi ya pili.

Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya Kocha Tite.

Paraguay, wapo chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi nne kuchezwa.

Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa kwa kichapo cha goli 2-0 na Bolivia na kushuka hadi nafasi ya 5, pointi moja nyuma ya Chile.

Uruguay, waliochapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wapo nafasi ya tatu.

Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za mtoano (nyumbani na ugenini) dhidi ya taifa moja kutoka Oceania.
Brazil ndio taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 Brazil ndio taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/29/2017 04:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.