Loading...

FIFA yamfungia Lionel Messi mechi 4 baada ya kumkuta na hatia ya kumtukana mwamuzi

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi amefungiwa kuichezea timu yake ya taifa kwa mechi nne.

Messi amefungiwa baada ya kumtukana mwamuzi katika mechi dhidi ya Chile ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.



Shirikisho la Soka la KImataifa (Fifa), limewataarifu Argentina ikiwa ni saa sita tu kabla ya kuivaa Bolivia katika mechi muhimu ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

Messi amepatikana na hatia ya kumtukana mwamuzi wa pembeni, Marcelo van Gasse akimtukana yeye na kumtukania mama yake.

Messi ndiye aliyefunga bao pekee lililoipa Argentina ushindi huo wa bao 1-0.
FIFA yamfungia Lionel Messi mechi 4 baada ya kumkuta na hatia ya kumtukana mwamuzi FIFA yamfungia Lionel Messi mechi 4 baada ya kumkuta na hatia ya kumtukana mwamuzi Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 08:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.