Loading...

Hali ya ukame Mkoani Manyara yasababisha mifugo zaidi ya 4000 kufa

Mifugo zaidi ya 4,000 ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imekufa kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame ulioikumba wilaya hiyo.

Wakizungumza juzi kuhusiana na tatizo hilo, wafugaji hao walidai kuwa ukame uliozikumba sehemu mbalimbali wilayani humo umesababisha mifugo yao ikiwamo ng’ombe, mbuzi na punda kufa.

Alex Mollel mmoja kati ya wafugaji hao alisema yeye binafsi amepoteza zaidi ya ng’ombe 250 kutokana na ukame na wafugaji wengi pia wamepata hasara kutokana na ukame huo ambao haujawahi kutokea.

“Huu ukame wa kipindi hiki umetusababishia hata bwawa la Kidawashi kukauka na pia mifugo imekosa maji na malisho hali inayosababisha hasara kubwa kwa wafugaji wengi,” alisema Mollel.

Alice Laizer alisema wingi wa mifugo umesaidia wafugaji wengine kubaki na baadhi ya mifugo baada ya mingine kufa, kwani endapo wangekuwa na mifugo michache, wengi wao wangeishiwa mifugo yote.

“Mfano kina Orenji walikuwa na ng’ombe 2,500 na hao 500 wakafa hivyo wamebaki ngombe 2,000 na baada ya miaka miwili au mitatu hiyo iliyobaki itazaana na kurudia idadi ya awali,” alisema Laizer.
Hali ya ukame Mkoani Manyara yasababisha mifugo zaidi ya 4000 kufa Hali ya ukame Mkoani Manyara yasababisha mifugo zaidi ya 4000 kufa Reviewed by Zero Degree on 3/01/2017 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.