Loading...

Hassan Kessy aeleza jinsi benchi la Yanga lilivyotaka kumkatisha tamaa

BEKI wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy, amesema kipindi kile ambacho alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, alipunguza mazoezi yake binafsi kwa kile alichokuwa anaona ni kujichosha wakati akiwa hapewi nafasi.

Hivi karibuni Kessy alirejea kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina baada ya kusota kwenye benchi muda mrefu kabla ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na nyingine mbili za kimataifa za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zanaco.
“Nilikuwa nafanya mazoezi kujiweka sawa lakini ilifikia muda nikapunguza kufanya kutokana na kuwekwa benchi ikiwa naweza kucheza na siyo majeruhi.”,Maneno ya 
Hassan Kessy.

“Ninahitaji kujiongezea fiziki katika kipindi hiki ambacho tayari nina nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ili kuisaidia timu yangu,” alisema Kessy.

Aidha mchezaji huyo wa zamani wa Simba amesema alichopanga hivi sasa kila siku atakuwa anafanya mazoezi ya binafsi ya gym na kukimbia barabarani kwa ajili ya kurejesha fiziki yake iliyopotea.

Source: ShaffihDauda
Hassan Kessy aeleza jinsi benchi la Yanga lilivyotaka kumkatisha tamaa Hassan Kessy aeleza jinsi benchi la Yanga lilivyotaka kumkatisha tamaa Reviewed by Zero Degree on 3/19/2017 12:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.