Loading...

Hatimaye Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wasaini mkataba mpya Simba SC

Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe unaweza ukasema amecheza kama Pele mara baada ya kukamilisha mipango ya usajili kwa Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wachezaji waliokuwa wanaelekea mwisho mwa mikataba yao.

Wawili hao mikataba yao ilikuwa inaisha mwishoni mwa msimu huu lakini wamekubali kuongeza mikataba ya miaka miwili kila mmoja.

Kwenye mikataba yote ya wachezaji hao, kila mchezaji anaruhusiwa kwenda kufanya majaribio kwenye klabu itakayoomba mchezaji husika kufanya hivyo na kuhama kama taratibu zitafuatwa.

Hii Ni Habari nzuri kwa wapenzi wa klabu ya Simba kwani wachezaji hao ni nguzo kubwa klabuni hapo kwasasa.
Hatimaye Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wasaini mkataba mpya Simba SC Hatimaye Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wasaini mkataba mpya Simba SC Reviewed by Zero Degree on 3/16/2017 12:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.