Loading...

Alichosema Conte kwa Jose Mourinho kwenye mechi ya FA ya Man U dhidi ya Chelsea chabainika

Macho yote yalikuwa juu juu, kama uliweza kushuhudia jinsi Kocha wa Chelsea Antonio Conte alivyokuwa akilalamikia kitu kwa Kocha wa Manchester United Jose Mourinho.

Kama ilivyobainika Conte alikuwa akipiga kelele za 'tena, tena, tena, tena' kwa Jose Mourinho inayohusiana na kiasi cha rafu nzito ambazo wachezaji wake walikuwa wakifanyiwa na kisha baadaye alifuatisha kauli nyingine na kusema kuwa 'chezeni mpira'.

Conte alikiri kutofurahia mbinu za mchezo wa nguvu tupu bila ustaarabu ulionyeshwa na United, hasa wakati wa kukabili Eden Hazard.

"Katika dakika 20, au 25 kwa Hazard, ilikuwa vigumu kwa yeye kucheza mpira," alisema kocha huyo wa Chelsea.


"Mimi naona tu kwamba yeye alipata nafasi ya kupigwa mateke tu. Sidhani kwamba mimi ni kipofu kiasi cha kumuona yeye peke yake katika hali hii.

'Alianza kwa mateke na kumaliza kwa mateke. Hakuna mtu anayeweza kusema hili halikutokea."

Alichosema Conte kwa Jose Mourinho kwenye mechi ya FA ya Man U dhidi ya Chelsea chabainika Alichosema Conte kwa Jose Mourinho kwenye mechi ya FA ya Man U dhidi ya Chelsea chabainika Reviewed by Zero Degree on 3/16/2017 01:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.