Loading...

Huyu ndiye straika anayetisha sana niliyekabiliana naye katika Ligi Kuu msimu huu, Gary Cahill

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hadi sasa amefunga hat-trick mbili katika michezo yake minne iliyopita kwenye kikosi cha Mauricio Pochettino cha Spurs na tayari Gary Cahill amemwelezea Harry Kane kama 'mshambuliaji hatari sana'.

"Kwa suala la washambuliaji katika ligi kuu, Harry Kane ndiye mshambuliaji ambaye unapaswa kuwa na hofu naye kwa sana kwani yuko kwenye kiwango cha juu.

Beki wa Chelsea, Garry Cahill akikabiliana na Harry Kane wa Tottenham
"Tumefanya mazoezi pamoja na ana uamaliziaji wa ajabu sana.

"Nadhani unasahau jinsi gani alivyo mdogo kiumri, ni mmaliziaji wa ajabu kwa kweli.

Harry Kane [Tottenham] akishangilia bao aliloshinda katika moja ya michezo ya Ligi kuu ya Uingereza
"Nadhani ameonyesha uwezo wake zaidi katika misimu kadhaa iliyopita mfululizo kwa kucheza katika kiwango cha juu na kuzalisha magoli kwa timu yake, kusema kweli yeye ni mmaliziaji mkubwa."

Cahill aliongeza: "Yeye ni mshambuliaji hatari sana, [lakini] sawa na [Zlatan] Ibrahimovic na [Sergio] Aguero ni washambuliaji ambao wako juu vile vile, n wachezaji ambao unapaswa kuwa makini nao kama beki."
Huyu ndiye straika anayetisha sana niliyekabiliana naye katika Ligi Kuu msimu huu, Gary Cahill Huyu ndiye straika anayetisha sana niliyekabiliana naye katika Ligi Kuu msimu huu, Gary Cahill Reviewed by Zero Degree on 3/11/2017 10:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.