Loading...

CCM ni kusuka au kunyoa leo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kinafanya vikao viwili vikubwa kwa mkupuo vya Kamati Kuu (CCM) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mkoani Dodoma.

Vikao hivyo vitafanyika kwa siku moja, baada ya Kamati Kuu kutofanyika jana. Badala yake siku nzima ya jana, ilitumika kwa ajili ya kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya chama.

Kikao hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili cha jana, kiliangalia maadili ya wanachama wake na kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais John Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho hujadili nidhamu za viongozi na baadhi ya wanachama waliokwenda kinyume na maadili ya chama hicho.

Kamati hiyo huhoji wanachama na viongozi na mapendekezo yake, hupelekekwa Kamati Kuu kwa ajili ya hatua zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema, vikao hivyo vitafanyika leo, ambapo Kamati Kuu itakutana asubuhi.

Alisema baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake, mchana Halmashauri Kuu itafanya mkutano wake, ambao ndio utakaoandaa ajenda kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, utakaofanyika kesho, ambao utafanya mageuzi makubwa katika chama.

Baadhi ya mageuzi hayo ni kubadilisha Katiba na Kanuni za chama pamoja na jumuiya zake, ikiwemo kupunguza wajumbe wake ili kuwa chama cha ufanisi zaidi.

Polepole aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote nchini, kuwasili mjini Dodoma na kuhudhuria kutokana na maandalizi yake kukamilika.

“Nawaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wafike mjini Dodoma kutokana na maandalizi yote kukamilika ili kufanikisha mkutano huo ambao ni muhimu katika kufanya mageuzi katika chama,” alisema Polepole.

Source: Habari Leo
CCM ni kusuka au kunyoa leo CCM ni kusuka au kunyoa leo Reviewed by Zero Degree on 3/11/2017 10:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.