Loading...

Jopo la Makardinali wapanga kumshinikiza Papa ajiuzulu kwa kukiuka maadili ya kanisa

Papa Francis I 
Jopo la Makardinali waliompa ushirikiano mkubwa Papa Francis wakati wa uteuzi wake, wamepanga kumshinikiza ajiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kanisa.

Gazeti la The Times na Libero la Italia, yameandika kuwa Makardinali hao zaidi ya dazeni, wamepanga kumshinikiza Papa Francis ajiuzulu lakini bila kujitenga naye kwa namna yoyote ile. Hata hivyo haijafafanuliwa ni maadili gani aliyoyavunja Papa huyo.

Makardinali hao ndiyo waliofanya jitihada kubwa za kuteuliwa kwa Papa Francis katika uteuzi wa nafasi hiyo mwaka 2013.

Mwandishi Antonio Socci ameandika katika gazeti la Libero na kueleza kuwa kwa sasa Makardinali wanajadili iwapo Papa akijiuzulu nani atashika nafasi yake.
Jopo la Makardinali wapanga kumshinikiza Papa ajiuzulu kwa kukiuka maadili ya kanisa Jopo la Makardinali wapanga kumshinikiza Papa ajiuzulu kwa kukiuka maadili ya kanisa Reviewed by Zero Degree on 3/03/2017 03:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.