Loading...

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC ateuliwa kurithi cheo cha baba yake

Felix Tshisekedi
Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo umemteua mwana wa kiume wabaliyekuwa kiongozi wa muungano huo Etienne Tshisekedi, ili kumrithi baba yake.

Felix Tshisekedi atakuwa rais wa muungano wa vyama tisa vinavyompinga rais Joseph Kabila.

Uteuzi wake ulitangazwa licha ya pingamizi kutoka kwa makundi mawili kwenye muungano huo.

Kiongozi wa muda mrefu wa muungano huo Etienne Tshisekedi, alikuwa ameuongoza kwenye mazungumzo ya mwezi Disemba kuhusu wadhifa wa urais.

Kwenye makubaliano yaliyoafikiwa, bwana Kabila ataondoka madarakani baada ya uchaguzi ambao utafanyika mwaka huu.

Muhula wake wa pili madarakani ulikamilika rasmi Disemba iliyopita.

Kifo cha bwana Tshisekedi kilizua ghasia za mwezi mmoja kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama mjini Kinshasa, na kusababisha taharuki ndani ya upinzani.

Tshisekedi alifariki mwezi mmoja uliopita
Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC ateuliwa kurithi cheo cha baba yake Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani DRC ateuliwa kurithi cheo cha baba yake Reviewed by Zero Degree on 3/03/2017 03:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.