Loading...

Jose Mourinho atabiri nafasi ya Zlatan Ibrahimovic kwenye tuzo za Ballon d'Or zijazo

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amemtabiria mchezaji wake, Zlatan Ibrahimovic kutwaa Tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu iwapo ataendeleza kasi ya kufunga mabao kwenye mechi atakazocheza msimu huu.

Kocha Mourinho alisema ana uhakika Ibrahimovic anastahili kunyakua tuzo hiyo na anaamini atakuwa miongoni mwa wachezaji waliotwaa tuzo hiyo katika umri wa miaka 35 akiwa Old Trafford.

Ibrahimovic amekuwa akifanya vyema katika mechi zote alizocheza tangu alipojiunga na Manchester United akitokea Paris Saint Germain, huku akizigusa nyavu mara 26 katika michezo yote 38 aliyocheza, kwenye mashindano mbalimbali na kutwaa Ngao ya jamii pamoja na Kombe la Ligi hivi karibuni.

Kocha huyo ambaye aliwahi kucheza nafasi ya mshambuliaji amempa nafasi kubwa ya kutwaa Tuzo ya Ballon d’Or hata hivyo, Mourinho amesema mwisho wa Messi na Ronaldo kutamba.
Jose Mourinho atabiri nafasi ya Zlatan Ibrahimovic kwenye tuzo za Ballon d'Or zijazo Jose Mourinho atabiri nafasi ya Zlatan Ibrahimovic kwenye tuzo za Ballon d'Or zijazo Reviewed by Zero Degree on 3/04/2017 04:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.