Loading...

Kauli ya Conte juu ya tetesi za kutaka kutimkia Inter, ...ataja tatizo pekee alilonalo Chelsea

Conte alifanya uamuzi wa kujiunga na Ligi kuu ya Uingereza kuja kuinoa 'The Blues', hata hivyo, familia yake bado haijaungana naye katika maisha yake mapya aliyoamua kuishi katika magharibi ya London.

Hata hivyo, wakati Conte amekiri kuwa ameukumbuka sana familia yake, muitaliano huyo anasisitiza kwamba maisha yake kwa muda mrefu anategemea atakuwa pale Stamford Bridge.

Alisema: "Tatizo kubwa kwangu mimi msimu huu ni juu ya kuikosa familia yangu hapa Uingereza kwa hakika, familia yangu ipo nchini Italia.

"Ninafanya kazi kwa ajili ya maisha ya baadaye na ili kujaribu kuwaleta wote hapa Uingereza kwa ajili yetu kuishi pamoja. Familia yangu imenikumbuka sansa kwa kweli. "

Alipoulizwa kuhusu uvumiwa kujiunga na klabu ya Inter, Conte Aliongeza: "Hali yangu ya kikazi iko wazi kabisa, mimi nina mkataba na Chelsea hayo mengine siyafahamu.

"Tunajaribu kujenga kitu muhimu kwa klabu, kwa sasa na baadaye. Hali iko wazi kabisa. "
Kauli ya Conte juu ya tetesi za kutaka kutimkia Inter, ...ataja tatizo pekee alilonalo Chelsea Kauli ya Conte juu ya tetesi za kutaka kutimkia Inter, ...ataja tatizo pekee alilonalo Chelsea Reviewed by Zero Degree on 3/04/2017 04:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.