Loading...

Kuelekea mechi ya Stars dhidi ya Burundi leo, ...Mavugo asema haya

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi ambaye anakipiga klabu ya Simba kwenye ligi kuu ya Tanzania Laudit Mavugo amesema timu yao imejipanga vizuri na ipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho March 28, 2017.

“Tumejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho na wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo,” anasema Mavugo wakati timu yake ilipofanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa taifa kuelekea mechi ya kesho.

Kuhusu kufahamiana na wachezaji wengi wa kikosi cha Stars ambao wanatoka Simba timu anayoicheza pamoja na wengine wa vilabu mbalimbali vya VPL, Mavugo amesema: “Ni changamoto kwangu kwa na kwao kwa sababu ninawajua na wao wananijua vizuri kwa hiyo tusubiri kesho nadhani utakuwa ni mchezo mgumu.”

“Utakuwa ni mchezo mgumu kwa sababu mara nyingi tumekuwa tunaifunga Stars, hata kesho tunaweza tukawafunga.”

Mavugo amesema mechi ya kesho huenda ikaendelea kupandisha hadhi yake endapo atafanya vizuri kama anavyotupia siku za hivi karibuni kwenye mashindano ya ligi kuu pamoja na Azam Sports Federation Cup.

“Ni kweli mchezo wa kesho unaweza kunipa au kunipunguzia sifa lakini kwa upande wetu tumejipanga vizuri.”

Mbali na hayo, nyota huyo kipenzi cha wanamsimbazi kwa sasa amesema, aliangalia game ya Stars vs Botswana na kusema wakicheza kama walivyofanya Jumamosi iliyopita huenda wakafanya vizuri.

Niliangalia mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Botswana japo niliangalia kipindi cha kwanza pekee lakini Stars walifanya vizuri, kama watajitahidi hata kesho wataweza kufanya vizuri pia.
Kuelekea mechi ya Stars dhidi ya Burundi leo, ...Mavugo asema haya Kuelekea mechi ya Stars dhidi ya Burundi leo, ...Mavugo asema haya Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 03:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.