Loading...

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyekuwa msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda, Andrew Felix Kawaeesi
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.

Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Andrew Felix Kawaeesi
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.

Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.

Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.

Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Reviewed by Zero Degree on 3/17/2017 11:53:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.