Hatimaye Mbwana Samatta afanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Europa
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji amekuwa Mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kushiriki hatua ya robo fainali ya Ligi ya Vilabu barani Ulaya maarufu kama UEFA Europa League.
Nafasi hiyo ambayo Samatta ameipata imekuja baada ya timu yake kutoka sare ya goli 1-1 na Gent katika mchezo wa marudiano wa hatua ya mtoano ya Europa League na hivyo kuiwezesha Tanzania kuingia katika vitabu vya kumbukumbu vya ligi hiyo kwa kuwa na mwakilishi.
Mchezo wa awali wakati timu hizo zilipokutana Genk iliibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Gent huku Samatta akifunga magoli mawili na hivyo sare ya goli 1-1 kufanya matokeo kuwa ni 6-3, ushindi ambao umeiwezesha Genk kusonga mbele.
Droo ya robo fainali inataraji kuchezwa ijumaa ya Machi, 17 kwenye makao makuu ya UEFA yaliyopo Nyon, Switzerland na timu ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ni Ajax (Uholanzi), Anderlecht (Ubelgiji), Besiktas (Uturuki), Celta Vigo (Hispania), Genk (Ubelgiji), Lyon (Ufaransa), Manchester United (Uingereza) na Schalke (Ujerumani).
Mchezo wa awali wakati timu hizo zilipokutana Genk iliibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Gent huku Samatta akifunga magoli mawili na hivyo sare ya goli 1-1 kufanya matokeo kuwa ni 6-3, ushindi ambao umeiwezesha Genk kusonga mbele.
Droo ya robo fainali inataraji kuchezwa ijumaa ya Machi, 17 kwenye makao makuu ya UEFA yaliyopo Nyon, Switzerland na timu ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ni Ajax (Uholanzi), Anderlecht (Ubelgiji), Besiktas (Uturuki), Celta Vigo (Hispania), Genk (Ubelgiji), Lyon (Ufaransa), Manchester United (Uingereza) na Schalke (Ujerumani).
Hatimaye Mbwana Samatta afanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Europa
Reviewed by Zero Degree
on
3/17/2017 11:44:00 AM
Rating: