Loading...

Msomi nchini Uganda afunguliwa mashtaka kwa komkosoa mke wa Rais Museveni

Bi Stella Nyanzi amewakosoa kwa pamoja rais Museveni na Mkewe Janeth Museveni kwa kushindwa kuwajali wasichana masikini wa Uganda
Msomi wa Uganda mwenye utata Stella Nyanzi ameitwa kwenye kituo cha upelelezi CID kujibu mashtaka ya "unyanyasaji wa kimtandao na matumizi mabaya ya kompyuta".

Bi Nyanzi ameshtakiwa baada ya kutuma ujumbe kadhaa kwa njia ya mtandao wa Facebook ambapo alisema mke wa rais wa Uganda Janet Museveni si "mama wa taifa " kama hawajali lolote kuhusu wasichana maskini wa Uganda ambao hushindwa kwenda shule ama kuacha masomo kwa kukosa visodo kwa ajili ya usafi wakati wa hedhi.

Bi Nyanzi ameshtakiwa baada ya kutuma ujumbe kadhaa wa Facebook ambapo alisema mke wa rais wa Uganda Janet Museveni si "mama wa taifa " iwapo ameshindwa kuwanunulia visodo vya hedhi wasichana masikini wa Uganda
Bi Museveni, ambaye pia ni waziri wa elimu nchini humo,kwa kawaida huitwa "Mama" ndani ya chama tawala na miongoni mwa vionguzi wa serikali

Bi Nyanzi, ambaye alitumia maneno makali na lugha ya aibu katika ukurasa aliandika katika ukurasa wake wa Facebook Jumatatu.

Mwezi wa wanawake umenifanya nizungumzie tena dhidi ya aibu ambayo Bi Janet Kataaha Museveni alitangaza katika bunge kwamba serikali ya Uganda haina pesa ya kutoa visodo vya hedhi kwa wasichana maskiniili wasikose kwenda shule wakati wa kipindi chao cha hedhi."

Katika ujumbe huo huo alimuelezea Bwana Museveni kama dikteta, akisema kuwa aliwadanganya masikini wa Uganda wakati wa kampeini zake za uchaguzi wa urais kujusu kuwapatia visodo mabinti zao".

Bi Nyanzi alikuwa mtafiti na mhadhili katika Chuo kikuu cha Makerere, na alifutwa kazi mwaka jana baada ya kutuma picha yake akiwa uchikupinga namna utawala wa chuo hicho ulivyomtendea.

Umati mdogo wa watu ulikusanyika mbele ya makao makuu ya CID katika mji mkuu, Kampala, kuonyesha kuwa wanamuunga mkono Bi Stella Nyanzi
Alirejeshwa tena kwenye chuo hicho mwezi uliopita.

Umati mdogo wa watu ulikusanyika mbele ya makao makuu ya CID katika mji mkuu , Kampala, kuonyesha kuwa wanamuunga mkono msomi huyo ,miongoni mwao akiwa mbunge MP Betty Nambooze.

Alisema kuwa anamuhusudu Bi Nyanzi Nyanzi kwa kuzungumza kwa niaba ya wasichana masikini wa Uganda na kwamba anapaswa kuzawadiwa na si kuhojiwa.
Msomi nchini Uganda afunguliwa mashtaka kwa komkosoa mke wa Rais Museveni Msomi nchini Uganda afunguliwa mashtaka kwa komkosoa mke wa Rais Museveni Reviewed by Zero Degree on 3/07/2017 06:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.