Loading...

Nape aunda tume kwa ajili ya kuchunguza uvamizi wa ofisi za Clouds uliofanywa na RC Makonda

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24.

Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ijumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.

“Matukio kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari,” alisema Nape


Aidha Nape amesema jambo lililotokea lisiwavunje moyo Clouds Media na wana habari kwa ujumla huku akisema kuwa serikali ipo kulinda haki za wanahabari bila kushinikizwa na lolote lililotokea.
Nape aunda tume kwa ajili ya kuchunguza uvamizi wa ofisi za Clouds uliofanywa na RC Makonda Nape aunda tume kwa ajili ya kuchunguza uvamizi wa ofisi za Clouds uliofanywa na RC Makonda Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 02:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.