Loading...

Nay wa Mitego akamatwa na polisi mkoani Morogoro

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva anayefanya sanaa yake tofauti na wasanii wengine, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego‘ inadaiwa amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akiwa Hotelini mara tu baada ya kumaliza kazi zake.

Msanii huyo amekuwa akiimba nyimbo zenye tungo tata na inadaiwa huwenda amekamatwa kutokana na wimbo wake mpya ‘Wapo’, unaosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Nay wa Mitego amedai amekamatwa na polisi wilayani Mvomero, Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show.

Hajasema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake Wapo ambao umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli. “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police,” ameandika rapper huyo mtata.

Ujumbe wake alioandika mitandaoni
Nay wa Mitego akamatwa na polisi mkoani Morogoro Nay wa Mitego akamatwa na polisi mkoani Morogoro Reviewed by Zero Degree on 3/26/2017 10:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.