Loading...

Njaa yaua watu 26 nchini Somalia

Watu 26 katika mkoa wa Jubbaland nchini Somalia wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana na kuwepo kwa njaa kali katika eneo hilo.

Watu hao wamepoteza maisha kutokana na hali ya ukame ambayo unalikabili taifa hilo jambo ambalo limesababisha wanyama kufa na mazao kukauka nakuwaacha wanancha watu milioni 6.2 bila chakula.

Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia, Mohamed Hussein amesema watu hao wamepoteza maisha katika kipindi cha masaa 36 yaliyopita na wengi wao wanakimbilia mji mkuu Mogadishu ili kupata msaada.

“Watu wa maeneo hayo wanahitaji msaada wa haraka sana,” alisema Hussein.
Njaa yaua watu 26 nchini Somalia Njaa yaua watu 26 nchini Somalia Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 10:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.