Loading...

FA kuiadhibu Manchester City kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake

Timu ya Manchester City, imeshitakiwa na chama cha soka cha nchini Uingereza FA, kwa kushindwa kuwathibiti wachezaji wake waliomzonga mwamuzi Michael Oliver, katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Man city, wanaweza pigwa faini kwa kosa hilo la wachezaji wake kwa tukio hilo lilitokea baada ya mwamuzi kuipa Liverpoool, penati.



Oliver alitoa adhabu ya penati baada ya kuona Gary Clichy, amemfanyia madhambi Roberto Frimino, katika eneo la hatari, na penati hiyo ikapigwa na James Milner aliyeukwamisha wavuni.

City wanatakiwa mpaka siku ya Alhamis kuwa wamepeleka utetezi wao kwa chama hicho cha soka cha Uingereza.

Mwamuzi Oliver alipatwa na kadhia kama hiyo ya kuzongwa na wachezaji wa Manchester united wiki iliyopita baada ya kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Ander Herrera katika mchezo wa kombe la FA kati ya Man United na Chelsea.
FA kuiadhibu Manchester City kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake FA kuiadhibu Manchester City kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 11:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.