Loading...

Alichosema Manara baada ya Yanga kupangwa na waarabu wa Algeria

Baada ya ratiba ya Caf Confederation Cup kuwekwa wazi na Yanga kutakiwa kucheza dhidi ya MC Alger ya Algeria, afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ame-post ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwatania Yanga kwamba mwisho wao kwenye michuano hiyo umefika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika: “Msiempenda kaja!! Kama nawaona vile Gongowazi (jina analotumia Manara siku za hivi karibuni kuwaita Yanga), safari imeshaiva hiyo na mwakani hammo.”


Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya MC Alger kati ya Aprili 7 hadi 9 kwenye uwanja wa taifa kabla ya kurudiana Aprili 13 hadi 15 nchini Algeria.

Kama Yanga itaitoa MC Alger, itafuzu hatua ya makundi ya michuano ya Caf Confederation Cup (CCC) 2017 ambapo msimu uliopita ilifika hatua hiyo ikiwa chini ya Hans van Pluijm lakini haikufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ya pili kwa ukubwa baada ya Caf Champions League (CCL).
Alichosema Manara baada ya Yanga kupangwa na waarabu wa Algeria Alichosema Manara baada ya Yanga kupangwa na waarabu wa Algeria Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 11:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.