Loading...

Rubani afariki dunia wakati ndege ikiwa safarini nchini Marekani

Rubani amefariki kwenye ndege iliyokuwa safarini kutoka Dallas kwenda Albuquerque huko New Mexico, kwa mujibu wa shirika la American Airlines.

Ndege hiyo aina ya Boeng 737-800, ilikuwa imesalia na karibu kilomita tatu kabla ya kutua, wakati nahodha alitangaza suala la dharura, kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege wa Albuquerque

Ndege hiyo ilitua bila ya kisa chochote na hakuna rubani aliyejeruhiwa.

Shirika la American Airlines lilimtaja rubani huyo kama William "Mike" Grubbs.

Mwaka 2015 rubani mwingine wa shirika hilo alifariki wakati wa safari kutoka Phoenix kuelekea Boston.

Ndege hiyo ilipelekwa na rubani mweza kwa njia iliyo salama hadi uwanja wa Syracuse mjini New York.
Rubani afariki dunia wakati ndege ikiwa safarini nchini Marekani Rubani afariki dunia wakati ndege ikiwa safarini nchini Marekani Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 06:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.