Kocha wa Burundi akiri kusikitishwa na kumkosa Samatta kwenye mechi ya juzi Taifa
KOCHA wa timu ya Taifa ya Burundi, Niyungeko Alain Olivier, amesikitika kukosa kumwona mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, katika mechi yao dhidi ya Taifa Stars, mchezo wa kirafiki uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Alain alisema alitarajia kumuona Samatta akiwa na kikosi chake cha Stars lakini ilishindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo.
Samatta aliondoka nchini hivi karibuni baada ya kuitumikia Stars kwenye mchezo wao dhidi ya Bostwana ambao unatambulika kwenye kalenda ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA), ambapo alifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 2-0.
Alain alitarajia timu yake kukutana na Samatta ili waweze kujifunza kitu kutoka kwake, kwani yeye ni mchezaji mkubwa anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Genk ya Ubelgij.
“Nilitarajia kumwona Samatta uwanjani ili angalau wachezaji wangu wajifunze kitu kutoka kwake, kwani yeye ni mchezaji mzoefu na anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya,” alisema Alain.
Samatta aliondoka nchini hivi karibuni baada ya kuitumikia Stars kwenye mchezo wao dhidi ya Bostwana ambao unatambulika kwenye kalenda ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA), ambapo alifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 2-0.
Alain alitarajia timu yake kukutana na Samatta ili waweze kujifunza kitu kutoka kwake, kwani yeye ni mchezaji mkubwa anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Genk ya Ubelgij.
“Nilitarajia kumwona Samatta uwanjani ili angalau wachezaji wangu wajifunze kitu kutoka kwake, kwani yeye ni mchezaji mzoefu na anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya,” alisema Alain.
Kocha wa Burundi akiri kusikitishwa na kumkosa Samatta kwenye mechi ya juzi Taifa
Reviewed by Zero Degree
on
3/30/2017 01:19:00 PM
Rating: