Loading...

Samatta kuikosa Burundi leo, ...hiki hapa kikosi kamili atakachoanzisha Mayanga

Kocha Salum Mayanga, amesema anaamini Taifa Stars watajituma ili kushinda mechi dhidi ya Burundi

Stars inaivaa Burundi katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

"Burundi ni timu ngumu, mara nyingi wana wachezaji wenye maumbo madogo lakini wenye vipaji.

"Lengo letu ni kufanya vizuri na wachezaji wanalijua hili. Kilichobaki ni kukumbushana na kuhimizana lakini tunachotaka ni kufanya vizuri," alisema.

Tayari Stars imeshinda mechi yake ya kwanza ya kirafiki chini ya Mayanga kwa kuichapa Botswana, Jumamosi iliyopita.
  1. Deo Munishi
  2. Shomari Kapombe
  3. Mohamed Hussein
  4. Abdi Banda
  5. Salim mbonde
  6. Himid Mao
  7. Simon Msuva
  8. Mzamiru Yassin
  9. Farid Mussa
  10. Abubakary Salum
  11. Ibrahim Ajib

Samatta kuikosa Burundi leo, ...hiki hapa kikosi kamili atakachoanzisha Mayanga Samatta kuikosa Burundi leo, ...hiki hapa kikosi kamili atakachoanzisha Mayanga Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 12:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.