Loading...

Simba SC yaanza mchakato wa kuondoa nyasi bandia bandarini, ..Kaburu atoa ufafanuzi juu ya hili

Baada ya kuwepo kwa taarifa ambayo inaelezea kuwa kampuni ya Majembe Auction Mart itapiga mnada nyasi bandia za Simba SC ambazo zipo bandarini, uongozi wa klabu ya Simba umejitokeza na kuzungumza kuhusu hatua ambayo wamefikia za kuondoa nyasi hizo.

Akizungumza na kituo cha redio cha E Fm, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu amekeri nyasi hizo kukaa bandarini kwa muda mrefu na baada ya serikali kukataa ombi lao la kupata msamaha wa kodi tayari wameshaanza taratibu za kulipa kodi ili kuziondoa bandarini.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu
“Ni kweli nyasi za bandia bado zipo bandari kavu ya Azam, baada ya kufika tuliwasiliana na Wizara ya Michezo na Wizara ya Fedha ili kuoma msamaha lakini pamoja na kufatilia kwa karibu sana Serikali ilikataa kutoa msahama wa nyasi hizi,” alisema Kaburu na kuongeza.

“Tulitarajia kuweka nyasi zile ni sehemu ambayo pia zitatumika kwa jamii sababu ya soka la vijana na sio kwa faida ya Simba peke yake lakini serikali ilikataa na tulifanya mpango mwingine wa kulipa kodi na tumeshawasiliana Kamishna wa Forodha na tulimwandikia barua ya kulipa kodi, kwa sasa wakala wetu anayeshughulia mizigo anafatilia ili kulipa kodi

“Kama hatua hizo zitatukuta zitatukuta tupo katikati ya mchakato lakini niwambie mashabiki wa Simba kwamba jambo hili tunalifahamu na tunalipa kipaumbele kwa sababu swala la uwanja wa Bunju kwetu sisi ni la kipekee, tunaamini tutafikia tamati ya jambo hili mapema inavyowezekana.”
Simba SC yaanza mchakato wa kuondoa nyasi bandia bandarini, ..Kaburu atoa ufafanuzi juu ya hili Simba SC yaanza mchakato wa kuondoa nyasi bandia bandarini, ..Kaburu atoa ufafanuzi juu ya hili Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 07:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.