Loading...

Taarifa muhimu kwa watumiaji wa simu za Iphone na Android

Mtandao wa WikiLeaks umetoa ripoti kuhusu CIA ku-hack watumiaji wa simu za Iphones na Androids Tarehe 7 March mwaka 2017, katika ripoti hiyo wamesema CIA wamekuwa wakiingilia mazungumzo binafsi ya watu wa kawaida wasiokuwa na madhara kwa taifa ambapo wamekua wakiona message binafsi kama WhatsApp.

CIA pia wame-hack simu zinazoingia na kutoka tangu mwaka 2013 hadi 2016, picha na kila kitu mtu anachofanya kwenye simu yake ya Androids na Iphones, ripoti hiyo pia imeishutumu CIA ku-hack TV aina ya Samsung kwa kuweka kifaa kinacho rekodi mazungumzo binafsi hata kama TV ikiwa imezimwa.

Wamiliki wa kampuni za Iphones na Androids wanaendelea kuchunguza taarifa hiyo iliyoogopesha watumiaji wa simu za aina hiyo, kwani taarifa ya kichunguzi inasemekana CIA wanafuatilia pasipo makampuni ya utengenezaji wa simu hizo kujua.
Taarifa muhimu kwa watumiaji wa simu za Iphone na Android Taarifa muhimu kwa watumiaji wa simu za Iphone na Android Reviewed by Zero Degree on 3/09/2017 01:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.