Tambwe, Ngoma waivuruga Yanga
WAKATI kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kikitarajia kuingia kambini Jumatano kujiandaa na mechi dhidi ya Azam FC, hali ya kutoimarika kiafya kwa washambuliaji wake tegemeo kunawaumiza 'kichwa'.
Washambuliaji hao ni Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao bado ni majeruhi.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema Ngoma na Tambwe bado hawajapona na kwa sasa hawako katika mipango ya kuwatumia kwenye mechi dhidi ya Azam FC itakayopigwa Jumamosi.
Mwambusi alisema kuwakosa washambuliaji hao wawili, kumerudisha nyuma kasi ya Yanga katika idara ya ushambuliaji na kusababisha kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu huyo aliongeza kuwa wataanza mazoezi, lakini hawatakuwa na uwezo wa kucheza mechi hiyo ambayo ina ushindani na yenye kutoa taswira ya bingwa wa msimu huu.
"Mechi yetu dhidi ya Azam ndiyo itatoa sura ya kutetea ubingwa tunaoushikilia, ni mechi ngumu lakini tunahitaji kupata pointi muhimu," alisema Mwambusi.
Alimtaja Geofrey Mwashiuya kuwa ameshapona na anatarajia kuingia kambini kuungana na nyota wengine wa timu hiyo kwa ajili ya kujifua na kuwa tayari kuwakabili mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi.
Baada ya mechi hiyo, Yanga itaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuwakaribisha MC Alger kutoka Algeria katika mechi ya kwanza ya mtoano kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbio za kuwania ubingwa wa ligi bado ziko wazi na katika msimamo wa mahasimu wao, Simba ndiyo wanaongoza wakiwa na pointi 55 wakati wao wakifuata kwa pointi 53.
Yanga ambayo ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye michuano ya kimataifa, waliangukia katika michuano hiyo baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia katika kinyang'anyiro cha kusaka taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOurce: Nipashe
Tambwe, Ngoma waivuruga Yanga
Reviewed by Zero Degree
on
3/26/2017 05:00:00 PM
Rating: