Loading...

Tanzania, China zasaini mkataba wa utamaduni

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamhuri ya watu wa China Dong Wei wamesaini programu ya utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba huo una lengo la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa Julius K. Nyerere.

“Tanzania na China tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo hili la Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu kuwa kitu kimoja”, Alisema Nape

Kwa upande wake Waziri Wei amesema ushirikiano kati ya Tanzania na China ulikuwepo kwa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni, Sanaa, Elimu,Ngoma na Michezo.

“Ushirikiano wetu wa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni umeleta mafanikio makubwa ambayo sote tunajivunia kila tunapokuwa pamoja”.Alisema Wei.
Tanzania, China zasaini mkataba wa utamaduni Tanzania, China zasaini mkataba wa utamaduni Reviewed by Zero Degree on 3/22/2017 11:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.