Loading...

Tanzania yashika nafasi ya 6 kwenye mashindano ya mbio za Dunia za nyika nchini Uganda.

Timu ya Taifa ya riadha iliyo kwenda kushiriki mashindano ya mbio za Dunia za nyika nchini Uganda imerejea nchini Tanzania, ilipeleka timu tano, nne kati yake zimeingia kumi bora huku moja ikishika nafasi ya sita kati ya zaidi ya nchi sabini zilizoshiriki mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa Chama cha riadha nchini Willihem Gidabudai amesema wanariadha wa Tanzania wameonesha uwezo mkubwa kwenye mashindano hayo huku Meneja wa timu ya taifa ya riadha akieleza umuhimu wa nafasi hiyo kwa Tanzania.



Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha riadha Zanzibar Makame Mshimba Mbaruku amesema walitegemea kurudia na medali nyingi katika mashindano hayo lakini kumekuwepo na changamoto kadhaa ambazo wamejifunza kutoka na makosa hayo.

Naodha wa timu hiyo Phabian Joseph naye akifikisha maombi yao kwa serikali na wadau wa michezo kuutunza mchezo wa riadha.
Tanzania yashika nafasi ya 6 kwenye mashindano ya mbio za Dunia za nyika nchini Uganda. Tanzania yashika nafasi ya 6 kwenye mashindano ya mbio za Dunia za nyika nchini Uganda. Reviewed by Zero Degree on 3/29/2017 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.