Loading...

Tanzania yashika nafasi ya pili kwenye matumizi ya Teknolojia katika Bara la Afrika.

Tanzania imeshika nafasi ya pili kati ya nchi arobaini na nne zinazopiga hatua kwenye matumizi ya teknolojia katika shughuli za maendeleo barani Afrika hali iliyotokana na watanzania kupata mwamko mkubwa wa kutumia teknolojia katika shughuli za maendeleo ya kila siku.

Kauli hiyo imesemwa na watalaam wa masuala ya sayansi na teknolojia katika uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya teknoljia katika shughuli za maendeleo iliyofanyika kwenye taasisi ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela ambapo katika ripoti iliyo zinduliwa nchini Senegal inaonesha Tanzania imeshika nafasi ya pili ikitanguliwa na nchi ya Moroco.

Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati Tanzania Emmanuel Kisongo,amesema tafiti pia zinaonyesha kuwa bara la Afrika bado liko nyuma katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na watu wake ukilinganisha na nchi zilizoendelea.

Mratibu wa Mradi unaosimamia tafiti hizo kutoka shirika la African Capasity Building Foundation (ACBF) la nchini Zimbabwe,Dkt.Michael Haule amesema Tanzania kupitia taasisi ya Nelson Mandela imeweza kunufaika na mradi huo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.
Tanzania yashika nafasi ya pili kwenye matumizi ya Teknolojia katika Bara la Afrika. Tanzania yashika nafasi ya pili kwenye matumizi ya Teknolojia katika Bara la Afrika. Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 06:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.