Loading...

TANZIA: Sir George Kahama Afariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama amefariki dunia jioni ya leo alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mwanasiasa, mwanaharakati na mpigania uhuru mahiri nchini Tanzania, Sir George Kahama (88), amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Habari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, John Steven, Kahama amefariki leo majira ya saa 10 jioni, huku maradhi yaliyosababisha kifo chake yakiwa bado hayajawekwa wazi.

Enzi za uhai wake, Kahama amewahi kuwa Waziri wa mambo ya Ndani wa Tanganyika (1961- 1962) na alikuwa msaidizi wa karibu wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mara ya mwisho, Kahama alionekana kwenye majukwaa ya kisiasa akiwa na aliyekuwa akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Benard Membe.

Akizungumza kuhusu kifo hicho, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), John Stephen alisema Sir Kahama alifariki saa 10:40 jioni alipokuwa akiendelea na vipimo katika kitengo cha dharura.

"Tulimpokea katika kitengo cha dharura Ijumaa na akalazwa hapa kwa kipindi chote alikuwa akiendelea na matibabu na wakati mauti inamfika alikuwa akipatiwa moja ya vipimo ambavyo alikuwa akiendelea navyo." alisema Stephen.





TANZIA: Sir George Kahama Afariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili TANZIA: Sir George Kahama Afariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Reviewed by Zero Degree on 3/12/2017 09:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.